Viongozi wa Dini mbalimbali wapatiwa chanjo ya Corona
NA THABIT MADAI, ZANZIBAR
VIONGOZI wa dini mbalimbali wamejitokeza katika zoezi la kupigaji wa chanjo ya Uviko 19 ili kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Viongozi hao walifika jana katika kituo cha upigaji wa chanjo hiyo kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja majira ya saa 5 asubuhi huku wakifuatana na waumini wao.
Akizungumza na waandishi wa habari mara ya kupatiwa chanjo hiyo, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Omar Kaabi, alisema, kujitokeza kwao ni kuunga mkono serikali ya kuwataka wananchi wake kujitokeza kwa hiyari kupata chanjo kwa hiyari.
Alisema endapo watakapo piga chanjo hiyo wataweza kuepukana na tatizo hilo, jambo ambalo dini inaipa kipaombele mtu kuendelea kujikinga.
Aidha alisema kujikinga nio bora kuliko tiba, kwani ukijikinga unajiepusha na maradhi yenyewe ambapo inaepusha pia harama wakati watatizo yashakufika.
“Tukijikinga tunaepusha harama hivyo, waumini wa dini zote tujitokezeni kwa wingi kwenda kupata chanjo ili kuweza kuepuka matatizo baadae” alisema.
Hivyo, alisema pamoja na hiyari viongozi hao ni mfano kwani wameonesha mkono jambo hilo na kuunga mkono chanjo ambapo msingi mkubwa ni kujikinga.
Hivyo, aliwataka waumini wote kwenda kufuata kinga hiyo kwani ugonjwa huo hauna dogo na maradhi hayo yamekuwa yaambukiza na wakijinga wataepuka kupata ugonjwa huo, sambamba na kufuata wataalamu wa afya ili taifa liweze kuwa na watu wenye afya bora.
Nae, Father Anselmo Mwang’amba, kutokea Parokia Kitope Zanzibar, alisema, aliona umuhimu wa chanjo na ndio akajitokeza kwenda kupiga chanjo hiyo na kuishukuru serikali kuweka chanjo hiyo.
Alisema alipofika alipatiwa chanjo hiyo bila ya usumbufu na kuwapongeza wataalamu wa afya wanaotoa chanjo hiyo kwani waliweza kumuhudumia vizuri.
Hhivyo waliwataka wananchi wengine waliokuwa tayari kujitokeza kwa wingi kuchanjwa, pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari inayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko ili kuepukana na maradhi hayo.
Nae, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Hassan Othman Ngwali, alisema wakifika katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa lengo la kuchanja kwani itawasaidia kuwakinga katika maradhi ya Korona.
Aidha alisema kuwa kwa upande wake alichanja chanjo ya Jonso jonsi, na kuwataka watu kujiepusha na uvumi kwani madaraktari hawajasema kuwa chanjo hiyo haifai kwa mwanaadamu ambapo badala yake wamekuwa wakiwachanja ili kujiepusha na ugonjwa wa corona.
“Kama daktari kasema chanjo hii mbaya tunaweza kumfata ila kama sio daktari hatuwezi kumfata kwani hii ni kinga na tunayemfata ni daktari na daktari katwambia kuwa chanjo hiyo ni salama na ni kinga na sisi tunakubali kuwa ni kinga” alisema.
Hivyo, aliwawasisitiza wananchi kujitokeza kupiga chanjo ingawa ni hiyari kwani kwa upande wao wameona inafaa na ndio wakajitokeza kupiga chanjo hiyo.
Kwa Upande wake, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shekhe, Khalid Ali Mfaume, alisema, dini ya Kiislamu inawahimiza waumini wake kuendelea kuchukua tahadhari ambapo kuchanjwa huko ni moja ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa.
‘Pamoja kuchanjwa huko ni hiyari lakini vile vile kusitokezee hiyari ya mwengine kumuambukiza ugonjwa mwengine kwani maradhi haya ni ya kuambukiza hivyo pamoja na kuwa ni ya hiyari pia tusiambukizane” alisema.
Viongozi hao waliongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Omar Kaabi Omar Kaabi walipigwa chanjo aina ya Jonson jonson.
Comments
Post a Comment