Posts

Meli ya kubeba ndege Uingereza ya Queen Elizabeth yatia nanga huko Japan kwa mara ya kwanza

Image
  Meli ya kubeba ndege Uingereza ya Queen Elizabeth ilitia nanga huko Japan kwa mara ya kwanza. Kikosi cha maamlum na meli ya kubeba ndege ambayo ilisafiri kutoka Uingereza mnamo Mei, ilifika Yokosuka, kituo cha baharini cha Marekani kilichoko kusini mwa mji mkuu wa Tokyo. Kamanda wa Kikosi maalum Steve Moorhouse alielezea ziara hiyo katika ujumbe wake kwenye Twitter kuwa kama kujitolea kwa Uingereza "kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, uchumi na usalama katika Indo-Pacific" na "kuchukua uhusiano uliopo kwa kiwango kipya" na Japan. "Uwepo wa meli hizo ni mfano wa uungwaji mkono wa Uingereza kwa uhuru na usalama wa njia muhimu za kibiashara katika eneo hilo na mfumo wa kimataifa ambao utafaidisha nchi zote," Moorhouse alisema. Kikosi maalum kitaondoka Japan Septemba 9. Ripoti ya shirika la utangazaji la umma NHK ilisema kwamba ziara hiyo "itaimarisha uhusiano wa kijeshi wa nchi husika na Japan, ambayo Uingereza inaona kama mshirika wake wa karibu zaid...

Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais anena haya

Image
  Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema uwepo wa sera na sheria zinazoendana kati ya Tanzania bara na Zanzibar ni fursa ya kuongeza ufanisi na kufikia malengo ya taasisi hizo   Ameyasema hayo katika kikao cha mashauriano ya pamoja kati ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu na ujumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wenye lengo la kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu hasa katika sekta ya Watu wenye Ulemavu.   Dkt Shajak amesema katika kukuza ufanisi ni vyema kuimarisha uhusiano wa karibu uliokuwepo wa taasisi zote mbili kuzungumza lugha moja ya kiutendaji kwa vile kila upande una mafanikio na changamoto za kiutendaji lakini mwisho wa siku tunazungumzia mafanikio na maslahi ya Watanzania ya Watu wenye Ulemavu.   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Adam amesema lengo la ujio wao ni kujifunza kutoka pande zote mbili kwa kubadilishana uzowefu na kuangalia miongozo wapi panah...

LHRC yaomba marekebisho ya sheria ya makosa ya jinai

Image
  Kituo cha sheria na haki za binaadamu  nchini Tanzania kimesema sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo imefanyiwa marekebisho Mwaka 1985 kwa kuondoa kifungu kinachoipa mahakama kuu kutimiza maombi ya dhamana hata katika makosa yasiokuwa na dhamana imepelekea mtuhumiwa kupewa dhamana kama anapewa zawadi  badala ya haki. Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Kituo cha sheria na haki za binaadamu  nchini Tanzania Wakili Ana Henga, Mjini Morogoro Septemba 6, 2021 wakati akifungua  kikao kazi cha  wadau kwaajili ya kutoa wasilisho la ripoti ya makosa yasiyo na dhamana. Wakili Ana Henga amesema ni wakati muafaka wa nchi ya Tanzania kuweka maboresho ya mfumo wa dhamana kutokana na mfumo uliopo sasa kuminya haki za Binaadamu na kumuumiza mtu kimwili na kisaikologia. Aliongeza kuwa kituo cha sheria na haki za binaadamu (LHRC) kiliangalia mfumo wa utoaji haki ya dhamana hapa nchini kwa kipindi cha mwaka 1945 hadi 2021 kuwa sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1945,a...

Viongozi wa Dini mbalimbali wapatiwa chanjo ya Corona

Image
  NA THABIT MADAI, ZANZIBAR   VIONGOZI wa dini mbalimbali wamejitokeza katika zoezi la kupigaji wa chanjo ya Uviko 19 ili kujikinga na ugonjwa wa Corona.   Viongozi hao walifika jana katika kituo cha upigaji wa chanjo hiyo kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja majira ya saa 5 asubuhi huku wakifuatana na waumini wao.   Akizungumza na waandishi wa habari mara ya kupatiwa chanjo hiyo, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Omar Kaabi, alisema, kujitokeza kwao ni kuunga mkono serikali ya kuwataka wananchi wake kujitokeza kwa hiyari kupata chanjo kwa hiyari.   Alisema endapo watakapo piga chanjo hiyo wataweza kuepukana na tatizo hilo, jambo ambalo dini inaipa kipaombele mtu kuendelea kujikinga.   Aidha alisema kujikinga nio bora kuliko tiba, kwani ukijikinga unajiepusha na maradhi yenyewe ambapo inaepusha pia harama wakati watatizo yashakufika.   “Tukijikinga tunaepusha harama hivyo, waumini wa dini zote tujitokezeni kwa wingi kwenda kupata chanjo ili kuweza k...

Wapenzi wa Simba Lindi wahaha kutafuta jezi mpya, wajipanga kikamilifu kushiriki Siku ya Simba

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi. Vilio vya wanachama, washabiki na wapenzi wa timu ya soka ya Simba( Wenye nchi) vinasikika mjini Lindi pia. Baada ya jitihada za kupata jezi mpya za timu hiyo kugonga mwamba mara mbili. Akizungumza wakati wa mkutano wa wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba wa tawi la Mshikamano ambao ulifanyika jana mjini Lindi, katibu wa tawi hilo, Ibrahim Mwaya alisema kupata jezi mpya za Simba imekuwa ni kazi ngumu ambayo hawakuitarajia. Mwaya ambae maelezo yake yaliungwa mkono na mtunza hazina wa tawi hilo, Omari Mswahili alisema licha ya kuwepo fedha za kununulia jezi hizo lakini changamoto ni kupata. Kwani mahitaji ni makubwa. Alisema licha ya kutuma fedha Dar-es-Salaam, lakini aliyetumiwa akanunue alikutana na ugumu uliosababisha fedha hizo ambazo zinatosha kununua jozi za jezi takribani 200 zilireshwa. " Huyo mtu aliamua kurejesha, baada ya kukosa jezi kwenye maduka ya Vunjabei. Alikuta misururu mikubwa na mwisho akaahidiwa Jumatatu( leo) uhenda atapata,...

Prof Ndalichako awaonya waliopanga kufanya udanganyifu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi wa darasa la saba kuepuka udanganyifu katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi. Wanafunzi hao wanafanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi Septemba 8 hadi 9 mwaka huu ikiwa ni awamu ya kwanza tangu utaratibu wa elimu bila malipo uanze nchini. Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 baada ya kukagua ujenzi wa shule ya mfano inayojengwa katika kata ya Iyumbu jijini Dodoma. Ujenzi wa shule hiyo uliofikia asilimia 60 unagharimu Sh17.1 bilioni na unatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2022. Profesa Ndalichako amesema maandalizi ya mitihani hiyo imekamilika na vifaa pamoja na mitihani imeshasambazwa kwenye vituo. “Miaka miwili mitatu iliyopita kumeanza kuwa na vidalili dalili vya kuijaribu Serikali watu wamekuwa wakifanya udanganyifu katika mitihani. Naomba niwatadharishe kuwa Serikali iko imara na tutakuwa makini katika kuhakikisha mitihani inafanyika kwa kuzingatia t...

Wadau wa maendeleo wajitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi 'jogging'

WADAU wa maendeleo katika Jimbo la Ubungo na Kata ya Makurumla mkoani Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye mbizo za mwendo wa pole( Jogging)zilizoandaliwa kwa lengo la kuchangisha fedha kufanikisha ujenzi wa matundu ya vyoo kwa Shule za Msingi ndani ya Kata hiyo. Jogging hiyo imeandaliwa. na Diwani wa Kata hiyo Bakari Kimwanga ikiwa ni mkakati wake wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga matundu 170 ya vyoo kwa shule hizo na kupitia mbio hizo wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.milioni 20. Katika mbio hizo zaidi ya washiriki 1,500 wamejitokeza kuunga mkono jitihada za Kata ya Makurumla na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo katika Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam. Akizungumza wakati akihitimisha mbio hizo za kilometa 10 zilizoanza saa 12 asubuhi hadi saa tatu asubuhi ,Profesa Kitila amempongeza Diwani wa Makurumla kwa kuandaa jogging kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazokwenda kutumika kujenga ...